Uncategorised

Kamati Tendaji ya “Project ECHO” Tanzania, iliyo chini ya Wizara ya Afya, imekutana Dodoma leo katika kikao chake cha 12 cha mwaka kilichofanyika katika Hoteli ya Morena na kuwakutanisha wadau mbalimbali katika Sekta ya Afya wakiwemo wataalamu kutoka TAMISEMI, Wizara ya Afya, Wataalamu wa Maabara, wadau wa maendeleo katika sekta ya afya na wataalam kutoka mabaraza ya wataam (Professional councils), Chuo kikuu Mzumbe na wafadhili wa Mradi (CDC).

Kikao hicho kilifunguliwa na Mwenyekiti wa muda wa Kikao hicho Bi. Mary Mtui, Msajili wa Baraza la Wataalamu wa Maabara kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali.  Amesema, pamoja na mambo mengine kikao hicho, kimekusudia kujadili na kuweka mikakati ya namna ya kuongeza ushiriki wa wataalamu wa Afya katika mafunzo kwa njia ya mtandao “ECHO Platforms” pamoja na namna wataalamu wa afya wanavyoweza kupanda madaraja/vyeo kwa kushiriki kwenye mafunzo hayo ambayo yanatolewa kila wiki kupitia vituo 9 (hubs) na watoa huduma za afya kutoka katika vituo (Spokes) zaidi ya 349 vilivyofungiwa vifaa vya mafunzo nchi nzima wananufaika na mafunzo hayo.

Miongoni mwa mafunzo yanayotolewa kwa sasa ni pamoja na kliniki za “Adult HIV, Pediatric HIV, MDR TB, HVL, HIV LAB, Supply Chain na AMS/IPC ECHO”. Hadi kikao cha 12 cha mwaka cha Kamati ya Utendaji, inakadiriwa zaidi ya CPD pointi 1000 zimetolewa kwa watumishi wa afya ambao wamekuwa wakipata mafunzo kwa njia hiyo ya mtandao, huku zaidi ya watumishi na watoa huduma za afya 650 wakishiriki mafunzo nchini nzima kila wiki.

Kikao hicho kimeweka mikakati mingi ya kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa afya popote walipo kwa kupata mafunzo ya kina yatakayosaidia kuboresha huduma za afya katika vituo vyote vya Afya nchini, pamoja na kuongeza wigo wa mafunzo kwa kutumia vifaa vya kisasa kwa kushirikiana na wafadhili, ili uwekezaji huo uweze kuwa na tija katika utoaji huduma za afya kwa wananchi.

Wakichangia mkutano huo, wadau wamepongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya na Wadau wa maendeleo CDC kwa kuwekeza katika mfumo wa mafunzo kwa njia ya mtandao; na hivyo kuwajengea uwezo wataalamu wa Afya wakiwa mahali pa kazi.

Akieleza mikakati zaidi ya Wizara; Mratibu wa Project ECHO Tanzania Bw. Jacob Lusekelo amesema, Wizara inakusudia kupanua wigo wa mafunzo na usimamizi kwa kuanzisha “Super Hub” nchini ambayo itakuwa na uwanda mpana zaidi wa kutoa mafunzo, mwongozo na usimamizi kwa wataalamu wa huduma za afya (immersion training).

Kikao hicho cha siku moja kimehudhuriwa na mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Huduma za Afya (TAMISEMI), pamoja na viongozi wengine kutoka Wizara ya Afya, TAMISEMI, wawakilishi kutoka Mabaraza ya Kitaaluma Tanzania, Chuo Kikuu Mzumbe, MDH, THPS, MNH na NBTS.

 

Mkurugenzi Msaidizi wa Afya TAMISEMI, Dkt. Paul Chaote, akikabidhi kitabu cha mwongozo wa utekelezaji wa shughuli za mradi wa

ECHO Tanzania “ECHO Framework” kwa Mwenyekiti wa kikao Bi. Mary Mtui  (Msajili wa Baraza la Wataalamu wa Maabara) kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali.

Mwenyekiti Bi. Mary Mtui (wa kwanza kushoto), akiendesha kikao cha Kamati Tendaji ya Project ECHO Tanzania, Dodoma.

Katikati ni Mratibu wa Project ECHO Tanzania Bw. Jacob Lusekelo, ambaye pia ni katibu wa Kamati hiyo.

Kulia ni Dkt. Miraji Ally Chaih, Mshauri Mwandamizi wa Mradi wa ECHO kupitia CDC -  Mzumbe.

Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Kamati Tendaji ya Project ECHO Tanzania, wakifuatilia  majadiliano wakati wa kikao.

Wajumbe wa Mkutano wa Kamati Tendaji ya Project ECHO Tanzania, wakiwa katika picha ya Pamoja baada ya kuhitimisha kikao.

Walioketi katikati ni Mwenyekiti wa kikao Bi. Mary Mtui, kulia kwako ni Dkt. Mackfallen Anasel wa Chuo Kikuu Mzumbe na kushoto kwake ni Dkt. Paul Chaote, kutoka TAMISEMI.

 

 

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu, leo ameongoza kikao cha Kamati ya Uundeshaji Mafunzo ya Epidemiolojia  na Usimamizi wa Maabara (TFELTP), kilichofanyika Dodoma na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kukinga Magonjwa (CDC), Dkt. Mahesh Swaminathan.

Akifungua Mkutano huo, Mganga Mkuu wa Serikali amezungumzia umuhimu wa mafunzo ya Epidemiolojia na Usimamizi wa Maabara Tanzania, na kusisitiza umuhimu wa kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya ngazi zote, ili kuwezesha Taifa kuweza kukabiliana na changamoto ya maradhi ya milipuko pindi yanapotokea ili kuweza kuchukua hatua haraka.

 “Ni muhimu tunapotoa haya mafunzo katika ufuatiliaji na kutilia mkazo elimu sahihi ya ukusanyaji wa taarifa na ufuatiliaji wa magonjwa kwa wataalama wetu ili kama Taifa tuweze kuitikia kwa haraka changamoto za magonjwa ya mlipuko kiulimwengu” Alisisitiza

Aidha amewashukuru na kuwapongeza wafadhili CDC, kwa kuendelea kufadhili mradi mkubwa unaosomesha baadhi ya wataalamu wa Epidemiolojia na kuahidi Wizara kuendelea kushirikiana na wafadhili hao katika kuhakikisha wataalamu wengi zaidi wanazalishwa ili kufikia malengo ya Wizara ya kuwa na Wataalamu wa kutosha wa Epidemiolojia nchini hususani katika mikoa ya pembezoni. Pia, amesisitiza umuhimu wa ufuatiliaji na kuwepo kwa takwimu sahihi za wataalamu wote waliopatiwa mafunzo hayo, ili Serikali iweze kuwatumia pindi kunapotokea changamoto za milipuko ya magonjwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha CDC, Dkt. Dr. Mahesh Swaminathan, amesisitiza umuhimu wa Wizara kuanzisha mfumo wa utunzaji taarifa pamoja na machapisho mbalimbali zikiwemo Sera, ambazo ni matokeo ya kuwepo wataalamu wa Epidemiolojia na mafunzo ya Maabara nchini, ili kuwa rahisi  kwa watanzania kufuatilia na kuwepo kwa kumbukumbu za matukio.

Ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha mradi wa CDC unakuwa na tija na matokeo yaliyokusudiwa kwa Watanzania.

Mkutano wa 14 wa Kamati ya Uongozi ya Mafunzo ya Epidemiolojia na Usimamizi wa Maabara (FELTP) umefanyika katika ofisi za Wizaya Afya, Area D Dodoma na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa, Chuo cha Afya Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali yanayoshughulikia masuala ya Afya, Shirika la Afya(WHO)na Chuo Kikuu Mzumbe watekelezaji wa Mradi wa DCD, Unaofadhiliwa na Serikali ya Watu wa Marekani.

Mkutano huo umeazimia kuongeza wigo wa mafunzo na kuongeza wataalamu Zaidi ili kufikia malengo ya Shirika la Afya Duniani (WHO), yanayotaka katika kila watu 200,000 pawepo na walau mtaalamu mmoja wa Epidemiolojia. Kwasasa Tanzania ina jumla ya wataalamu 892 waliopatiwa mafunzo ya Epidemiolojia na Maabara walioajiriwa katika maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Nchi.

***************************************************************************

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu, akiongoza kikao cha Kamati ya Uendeshaji ya Mafunzo ya Epidemiolojia 

na Usimamizi wa Maabara (FELTP), kilichofanyika Dodoma.

Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha CDC, Dkt. Dr. Mahesh Swaminathan, akikabidhi zawadi ya kanga kwa Mganga Mkuu wa Serikali Prof.

Tumaini Nagu. Zawadi hiyo ni kanga ya maadhimisho ya miaka 20 ya PEPFAR.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Nagu akiagana na Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha CDC, Dkt. Dr. Mahesh Swaminathan.

 

Vijana Wasomi nchini Tanzania wametakiwa kuwa wabunifu na kutumia usomi wao kutatua tatizo la ajira kwa kuacha kufikiria zaidi kuajiriwa na Serikali au na makampuni makubwa na badala yake watumie fursa zinazowazunguka zikiwemo kilimo,viwanda na biashara ili kuweza kujiajiri na kujiatia kipato.

 

Hayo yamesemwa na Waziri wa ofisi ya Makamu wa Rais (mazingira na Muungano) Mh. Januari Makamba amewataka vijana na wasomi  wakati akifungua kongamano la majadiliano na kubadilishana fikra kwa vijana wasomi wa chuo kikuu mzumbe lililoandaliwa na jukwaa la vijana ‘Think Tank’ kwa lengo la kutambua fursa, mitaji na masoko.

 Alisema kuwa Serikali haiwezi kuajiri wasomi wanaohitimu kwenye vyuo vyote hapa nchini hivyo kuelekea uchumi wa viwanda vijana wasomi wanayo fursa ya kufanya shughuli mbalimbali za kujipatia  kipato kupitia sekta ya viwanda.

 Akitoa mada katika kongamano hilo Mkurugenzi wa vipindi na uendeshaji wa Clouds Media group, Ruge Mutahaba alisema kuwa wakati huu wa ulimwengu wa sayansi na teknojia lazima vijana wabadilishe fikra za kusubiri kuajiriwa na badala yake watafute maarifa ya kujiajiri.

 Mutahaba alisema kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda vijana wanayo nafasi nzuri ya kupiga hatua ya maendeleo kupitia sekta ya viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi na shughuli nyingine za ujasiliamali.

 Naye mratibu wa jukwaa la vijana Think Tank Suma Mwaitenda alisema kuwa jukwaa hilo linakusanya mawazo ya vijana ambao wamejitolea kuleta fikra mpya kwa ajili ya kuleta maelendeo.

 Alisema kuwa kila mwaka vijana wanaohitimu vyuo  mbalimbali hapa nchini ni  takribani 800,000 hadi 1,000,000 hata hivyo wanaopata ajira Serikalini na sekta binafsi ni asilimia 10 pekee, hivyo makongamano hayo yatasaidia kubadilisha fikra na kuwapa maarifa vijana ya kujiajiri na hatimaye kuisaidia serikali kutatua changamoto ya ajira na kukuza uchumi.

 Alivitaja vyuo watakavyofanya kongamano kama hilo kuwa ni pamoja na chuo cha tiba Muhimbili, Udom, Mtakatifu Agustino, shule ya sheria na Chuo Kikuu Dar es Salaam.

 Kwa upande wake mwanafunzi wa chuo hicho Asha Sungura alisema kuwa kongamano hilo limeweza kumsaidia kuongeza maarifa na ubunifu katika ujasiriamali wa kilimo cha zabibu anachofanya mkoani Dodoma.

 Alisema kuwa kongamano hilo limemsaidia kufahamu namna ya kuongeza thamani ya bidhaa anayozalisha pamoja na kutafuta mitaji na masoko hivyo aliwashauri wanafunzi wenzake kutokata tamaa na mitaji waliyonayo badala yake waanze na mitaji midogo ambayo itaongezeka.

 

 

 

 

FOURTH  CORPORATE STRATEGIC PLAN 2017/2018-2021/2022

 Download the Fourth Corporate Strategic plan 2017/2018-2021/2022 here.

News and Updates

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top